+255 712 345 678 info@fti.ac.tz Olmotonyi, Arusha - Tanzania
logo

Ministry of Natural Resources and Tourism

FORESTRY TRAINING INSTITUTE - OLMOTONYI

News and Events

  • Home
  • highlights
  • fti-kati-ya-vyuo-bora-duniani-mhe-angellah-kairuki
  • By Admin
  • News and Events

FTI kati ya Vyuo Bora Duniani -  Mhe. Angellah Kairuki

Chuo cha Misitu Olmotonyi (FTI) ni chuo pekee kikubwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 1937 na ni moja ya chuo bora kabisa kuwepo Afrika Mashariki, Afrika na Duniani, katika utoaji wa mafunzo ya misitu kwa nadharia na vitendo. Hayo yamesemwa Februari 5,2024 na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) alipofanya ziara ya kikazi katika chuo hicho kilichopo jijini Arusha. Chuo hicho kimekuwa kikitoa mafunzo ya misitu katika kozi za Astashahada ya awali ya misitu, Astashahada ya Misitu, Stashahada ya Misitu, Stashahada ya Misitu ya mijini na usanifu wa mandhari, stashahada ya jioinfomantiki katika usimamizi wa maliasili (Geoinformatics for Natural Resources and Management) pamoja na mafunzo ya muda mfupi ya misitu na uhifadhi wa mazingira.

Waziri Kairuki amesema ili kukikuza zaidi chuo hicho, Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii inaendelea kufanya mapitio ya mitaala yake kuhakikisha kwamba inaendana na mahitaji ya sasa ya kidunia katika taaluma ya ulinzi, usimamizi na uendelezaji wa misitu. Aidha, amesema Wizara itaendelea kuboresha mazingira ya chuo hicho ikiwa ni pamoja na kuangalia namna ya kuongeza karakana, mashine mpya, majengo mapya na maboresho mengine.